Varangati hilo lililonaswa na kachero wetu lilijiri wikiendi iliyopita maeneo ya Sinza- Afrika Sana jijini Dar.
Katika sinema hiyo ya bure, mrembo huyo alishuhudiwa akipigana na kila
mtu aliyekutana naye mbele yake huku akivua nguo kuashiria kuwa ‘pombe
si chai’.
Kuna wakati mwanadada huyo alikatiza barabarani bila kujali magari na
nusura agongwe jambo lililosababisha mtafaruku wa foleni huku mwenyewe
akidondoka kama ‘embe dodo’ lililoiva.
Baada ya timbwili hilo kuchukua takriban dakika 35, ilibidi wasamaria wema kuingilia kati na kumshika huku akiwapiga baada ya kuona huenda angeumizwa.
Baadaye watu hao walifanikiwa kumtoa eneo la barabara huku wakimsitiri
kwa kupandisha nguo kufunika nido kisha kumpeleka pembeni na kumtuliza.
“Kweli pombe siyo chai. Yaani msichana mzuri lakini ona alivyojidhalilisha,” alisema mmoja wa mashuhuda hao.
Source: Global publisher