Hatimaye
msanii mkongwe wa bongofleva hapa nchini Afande Sele amefunguka leo na
kusema kuwa hii leo anajiunga rasmi na CHADEMA, haya hapa chini ndiyo
maneno yake kupitia facebook account yake
"Hakuna
kusanda,hakuna kumbwanda,mbele kwa mbele makamanda,vua gamba vaa gwanda
kisha kaza mkanda, wanashuka sisi tunapandaaa,,,,
Leo
tunaanza kuandika historia mpya ktk mkoa wetu wa morogoro na tz kwa
ujumla kwa sababu nikiwa kama msanii wa muda mrefu na mfalme pekee wa
mzk wa kizazi kipya ninaetunga nyimbo zangu kwa kuzingatia ujumbe muhimu
ktk jamii kwa mambo ya kisiasa,kiuchumi,elimu,amani na upendo nk,
Sasa
leo nimeamua kwa ridhaa yangu iliyosukumwa na uzalendo na mapenz
makubwa kwa taifa langu kuchukua kadi ya kujiunga rasmi uanachama wa
CHADEMA,tukio hilo kubwa litafanyika leo jioni ktk mkutano wa hadhara
utakaofanyika kata yetu ya mafiga/misufini na utahudhuriwa na viongoz
mbalimbali wa chama kutoka makao makuu ya chama Dsm pamoja na mbunge wa
nyamagana mh Ezekiel Wenje,kwa wakaz wa Moro wazalendo nyote
mnakaribishwa saaana, ahsanteni wana'ndugu, siasa si uadui,
tupingane/tusipigane, Pendo moja!,,,