Search in This Blog

MTANDAO ANAOTUMIA JACK KWA AJILI YA UNGA NI NOMA, SOMA HAPA UONEMWENYEWE



Jack akiwa chini ya ulinzi baada ya kunaswa na dawa za kulevya China.
Na Mwandishi Wetu
BADO habari ya mjini ni skendo ya kunaswa na madawa ya kulevya ‘unga’ inayomtafuna Video Queen wa Bongo, Jacqueline Clifford Fitzpatrick ‘Jack Patrick’ ambaye inadaiwa kuwa mtandao wake wa biashara hiyo ni wa kutisha, Ijumaa limetonywa.

Jack Patrick.
Habari kutoka kwa rafiki wa karibu wa Jack ambaye aliomba chondechonde asitajwe, alidai kwa sasa vigogo wanaojihusisha na biashara hiyo haramu wamekuwa wakihaha kwa hofu kuwa modo huyo anaweza kuwataja hivyo wanafanya kila linalowezekana ili wamnusuru kama ilivyokuwa kwa Agnes Gerald ‘Masogange’.
Ilisemekana kuwa katika mtandao huo, vigogo hao wenye maskani jijini Dar, Rwanda, Uganda, Kenya, Dubai, Thailand, Italia na Hong Kong wamekuwa wakihaha kumuokoa Jack bila mafanikio.
“Unajua China siyo rahisi kumchomoa kama ilivyokuwa kwa Masogange (Agness Gerald) aliyenaswa Sauz (Afrika Kusini) kwa sababu wale (China) Tanzania haikuwasaidia kupata uhuru kama ilivyokuwa kwa Sauz.

Polisi wakichunguza pipi zenye dawa za kulevya alizokutwa nazo Jack Patrick.
“Ile ngoma ni mbichi, hakuna upenyo wa rushwa pale. Ngojeni tusubiri hukumu maana itakuwa kali sana, nazijua vizuri sheria za China juu ya madawa ya kulevya,” alisema rafiki huyo wa Jack na kuongeza:
“Hakuna ishu iliyoniuma kama ya Jack kwa mwaka uliomalizika.”
Katika nusanusa za gazeti hili, ilidaiwa kuwa bosi aliyemtuma Jack ni mwanamke mmoja tajiri aishie jijini Dar ambaye ana mtandao mkubwa wa biashara hiyo duniani.

Ili kuthibitisha kuwa mtandao uliodaiwa kumtuma Jack unatisha na una watu wazito, ilielezwa kwamba mrembo huyo hakuwa peke yake kwani alifuatana na warembo wawili, mmoja Mtanzania na mwingine raia wa Rwanda ambao wao walifanikiwa kuwatoroka polisi wa China.
Mbali na timu hiyo ya watu watatu waliokuwa na mzigo mwilini, pia kulikuwa na mtu mwingine aliyekuwa akiwasindikiza.
Ilidaiwa kuwa baada ya kupakia mzigo watu hao waliondoka Dar kupitia Nairobi, Kenya kisha Dubai ambapo walitua Bangkok, Thailand kabla ya kutimkia Macau, Hong Kong wakielekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China.
Ilisemekana kuwa sehemu zote hizo hawakushtukiwa kwa kuwa mtandao wao ni mkubwa na inaonekana ni wazoefu kwa shughuli hizo.
Kutisha kwingine kulikozungumziwa ni kiasi cha mzigo aliokuwa amebeba Jack wa kilo 1.1 za heroin wa zaidi ya Sh. milioni 200 kwa yeye peke yake bila kujua kiasi walichokuwa wamepakia wenzake.

“Kinachoonekana jamaa wana mtandao mkubwa maana ukicheki kiasi alichokutwa nacho Jack ni kikubwa mno,” alisema modo maarufu anayefanya kazi za mitindo na Jack.
Bado Jack yupo mikononi mwa polisi wa China tangu aliponaswa kwenye Uwanja wa Ndege wa Macau, China, Desemba 19, mwaka jana ambapo upelelezi wa awali unaendelea.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger