Dada wa Lucas Lomayany Molel (37) anayesakwa kwa kumuua mkewe wa ndoa, Agnes Lucas (24), akiwa katika chumba kilichotumika kwa mauaji hayo.
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linamsaka kwa udi na uvumba, muuza nyama jijini hapa, Lucas Lomayany Molel (37) mkazi wa Ilboru kwa madai ya kumuua mkewe wa ndoa, Agnes Lucas (24) kwa kumcharanga na sime kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.
Chanzo cha habari kimeliambia kuwa,
tukio hilo la kutisha lilitokea usiku wa kuamkia Julai 7, mwaka huu,
nyumbani kwa mtuhumiwa ambapo baada ya kutekeleza mauaji hayo aliufunika
mwili wa marehemu kwa shuka na kuendelea kulala nao kitandani hadi
alfajiri alipotoroka.
Akisimulia kuhusu mauaji hayo kwa
paparazi, ndugu wa marehemu aitwaye William Lomayany alisema usiku wa
tukio, saa 4, mtuhumiwa alirejea nyumbani kwake na kutomkuta mkewe,
akamsubiri hadi saa 6 usiku, mke akarejea.
Alisema marehemu baada ya kufunguliwa
mlango na kuingia, alivua nguo zote na kubaki na ‘kufuli’ ambapo
alijifunga kanga na kupanda kitandani kulala. Mtuhumiwa alimfuata
chumbani na kumhoji kuhusu kuchelewa nyumbani hadi muda huo na ndipo
mzozo ulipoanza.
William alizidi kusema kuwa, wawili hao
walianza kugombana kwa maneno lakini baada ya muda hali ya utulivu
ilirejea, ndipo asubuhi ilipopatikana taarifa za kuuawa kwa Agnes jambo
lililotafsiriwa kuwa huenda utulivu huo tayari Agnes alishauawa.
Inadaiwa kuwa, mtoto wa kwanza wa
mtuhumiwa, Jessica Lucas (11) ndiye aliyekuwa wa kwanza kufungua mlango
wa chumbani kwa wazazi wake na kumkuta mama yake amelala na damu
chapachapa, akaenda kutoa taarifa kwa majirani.
Ilidaiwa kuwa, baada ya taarifa hiyo,
majirani waliingia ndani ya chumba hicho na kuukuta mwili wa marehemu
ukiwa umelala kwenye dimbwi la damu huku akiwa mtupu.
Akizungumza mbele ya askari polisi
waliofika kushuhudia tukio hilo, Jessica alisema baba yake alimwamsha
usiku akimtaka atoke kufunga mlango baada ya kutoka ndani. Akajua baba
yake anakwenda kazini kama ada.
“Nilikwenda kufunga mlango, baba
aliondoka bila kusema chochote. Lakini jana usiku (Julai 6) baba
alimpiga sana mama na alinipiga na mimi wakati namwambia amsamehe,”
alisema Jessica.
Majirani wa wanandoa hao, wamelaani
mauaji hayo na kusema Lucas hakupaswa kumuua mkewe badala yake
angewashirikisha watu wengine wakiwemo wazazi wamkanye kama alikuwa
akimsaliti.
“Kwa jinsi Lucas alivyokuwa mpole sikutegemea kama angemuua mkewe kikatili, kama alikuwa akimsaliti angewaeleza wazazi wake ili wamkanye,” alisema jirani yao ambaye hakupenda jina lake liandikwe paparazini.
“Kwa jinsi Lucas alivyokuwa mpole sikutegemea kama angemuua mkewe kikatili, kama alikuwa akimsaliti angewaeleza wazazi wake ili wamkanye,” alisema jirani yao ambaye hakupenda jina lake liandikwe paparazini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,
Liberatus Sabas alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa,
uchunguzi unaendelea na jeshi lake linamsaka mtuhumiwa huyo.