Habari zinazo-make headlines hivi sasa kila kona ya media hapa town ni
tukio la mkali wa AfroPop Diamond Platnumz kumzawadia mama yake zawadi
ya gari aina ya Toyota Lexus, huku mama yake akiwa anatimiza miaka 55 ya
kuzaliwa kwake, Diamond Platnumz inasemekana ilimtoka kitita cha
shilingi milioni 38(38,100,000/-) kuweza kununua usafiri huo kama zawadi
kwa mama yake mzazi, ambapo mil.35 imetumika kulinunulia gari hilo
mpaka kuingia Tanzania na Milion 3.1 imetumika kulipamba na kuweka Music
System pamoja na seat Cover. .
Diamond Platnumz kwa bahati mbaya hakuwa katika eneo la tukio kutokana
na kuwa safarini huko marekani, ila mama yake alionekana kufrahi sana
hadi kutokwa na machozi kwa surprize hiyo, jambo lililomfanya Diamond
mwenyewe kufunguka na kusema kuwa chozi lilimtoka alipomuona mama yake
akiwa analia kwa furaha namna hiyo.Siku hiyo hiyo iliambatana na suprize
kwa fans wake kwa kudondosha pia video zake mpya mbili.