Rihanna haendeshwi na matukio na wala hatabiriki katika mitindo ya
mavazi anayochagua. Uamuzi wake mara nyingi huzua maswali na changamoto
kwa wengi.
Mwimbaji huyo wa kike ameonekana mtaani akiwa anapiga misele na vazi la
kulalia aka Night Dress na anaonekana akiwa anajiamini kama mtu aliyevaa
suti au nguo nyingine inayompasa kuzurura nayo katikati ya jiji.