Akichonga na paparazi wetu, Rose alisema wamerudi kwa staili ya tofauti kwani kila mmoja anafanya kazi zake lakini wanashirikishana na wana ‘project’ maalum ambayo wataifanya hivi karibuni.
“Mimi na Jack kwa sasa tunafanya kazi hata Wema ambaye tulikuwa naye kwenye kundi moja tukiwa na filamu ya kumshirikisha tutamuita kwa sababu hatuna kinyongo kwani bifu hazijengi kikubwa tunafanya kazi tu,” alisema Rose.
Staa wa filamu Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ kulia akiwa na Rose Ndauka.
Rose na Jack Chuz walipishana kipindi cha nyuma na chanzo kikidaiwa
kuwa ni kuibiana mabwana lakini hivi karibuni walimaliza tofauti ambapo
walionekana pamoja kwenye msiba wa aliyekuwa muongozaji wa filamu
nchini, George Otieno ‘Tyson’.