Moja
kwa moja niende kwenye maada. Mkasa huu umenikumba nikiwa nafanya kazi
mkoa flani kanda ya kati. Katika eneo ambalo nilikuwa naishi ni karibu
na sehemu ambayo baba yangu alikuwa anafanyia kazi kabla ya kustaafu na
kurudi nyumbani kwake namaanisha mkoa alikozaliwa yeye ambao upo kusini
nyanda za juu.
Wakati
baba anastaafu na kurudi mkoa aliozaliwa mimi na nikabaki mkoa huo huo
aliokuwa anafanya kazi sikuweza kuhama naye kwasababu nilikuwa nafanya
kazi kwenye kampuni moja ya mawasiliano .
Katika
kipindi alichokuwa anafanya kazi kumbe alizaa nje ya ndoa na mwanamke
mmoja lakini baba hakuweza kumhudumia yule mtoto kitendo ambacho
kilimfanya mama mtoto asimweke karibu na baba.
Hata
yeye baba hakuwahi kutuambia kuwa aliwahi kuzaa nje ya ndoa. Katka
kipindi chote hicho mama huyo na mwanaye walikuwa wakiishi mbali kidogo
na wilaya yetu.
Basi
katika mizunguko ya kazi hapa na pale nilikutana na dada huyu ambaye
ndiye nimezaa naye pasina kujua ni dada yangu. Tulikutana kwenye semina
mkoani Kilimanjaro kama ilivyo kawaida ya wanaume nikamuaproach yule
dada na akaingia line. Tukaanza kujihusisha kimapenzi kwa muda wa mwaka
mzima mpaka alipopata ujauzito.
Ikanilazimu
niukubali ule ujauzito na nikatafuta wazee wa mtaa ninaokaa na kwenda
nyumbani kwa mwanamke ili kujitambulisha. Yule mama mkwe ambaye ni mama
mdogo kihalali alipoona majina yangu matatu akapatwa na wasi wasi japo
barua ilipokelewa.
Ikabidi akanitafuta kwa kuniuliza kiundani nilipojieleza ndipo akasema huyu uliyempa mimba ni dadayako tena wa damu.
Kwakweli
niliishiwa nguvu akaanza kunisimulia kila kitu kuhusu baba yangu. Mpaka
hapa ninapo andika mwanamke ameshajifungua na mtoto ana miezi 5.
Baba sijamwambia bado ila nataka nimpeleke huyu binti nyumban kwetu. Na hii siri naijua mimi na mama mkwe au mama mdogo.
Sijajua nifanyeje mama mwenyewe ameshindwa afanye nini, tunaogopa kuwashirikisha watu aibu.