Tayari alikuwa ameweka mizizi huko Nollywood, Nigeria, Gollywood, Ghana, Hollywood, Marekani, Uingereza, Rwanda, Burundi, Congo na sehemu nyingine duniani. Kuna ushahidi kuwa alikuwa amesaini mkataba wa kufanya filamu huko Hollywood ambayo ingempa utajiri mkubwa kuliko staa yeyote Afrika Mashariki. Kibaya aliondoka mapema kwa kuwa kizuri hakidumu. Kama Kanumba angekuwa hai, naamini filamu za Kitanzania zingekuwa mbali sana kimataifa.
Usiku wa kifo cha Kanumba haukuwa mzuri hata kidogo kwa watu wengi. Habari zilisambaa kama moto wa kifuu hasa kupitia mitandao ya kijamii, vyombo vya habari na simu za mkononi. Kila mtu alibisha. Wengine walidhani ni sehemu ya filamu zake. Hata hivyo, baadaye madaktari wa Muhimbili walithibitisha kifo chake. Kibaya zaidi, kifo chake kilihusishwa na mwigizaji kinda, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye alikamatwa na kuwekwa katika Mahabusu ya Segerea, Dar kabla ya hivi karibuni kutoka kwa dhamana na kesi inatarajiwa kuanza kuunguruma muda wowote.
Kanumba alipendwa na bado anapendwa majumbani hasa wanawake na watoto. Kilipotangazwa kifo chake mwanamke mmoja alikunywa sumu huko mkoani Pwani. Watoto walimlilia kwa sababu ya aina ya filamu alizoigiza zilizogusa maisha yao. Alikuwa kipenzi cha watoto.
Usiri wa maisha binafsi, hata lile la uhusiano wake na Lulu, upembuzi wa mambo, kujituma katika kazi, ushawishi, kutokuwa na majivuno na upole, ni vitu vinavyoigwa kutoka kwake hasa na wasanii wenzake.
Kuanzia akiigiza tamthiliya akiwa Kaole Sanaa Group hadi akaingia kwenye filamu, nyota yake ilikuwa iking’aa hata kama kipato hakikuwa kikubwa. Msanifu kurasa wa Global Publishers, Huruma Bujiku huwa analengwalengwa na machozi kila anapotengeneza kurasa zinazohitaji matumizi ya picha za Kanumba.
No comments:
Post a Comment