Search in This Blog

TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA BARABARA YA MTWARA - LINDI KWENDA MASASI, NACHINGWEA, LIWALE NA RWANGWA

Na Mdau Abdulaziz Video
Abiria wanaosafiri kati ya Mtwara na Lindi kwenda Masasi na watokao Masasi Tunduru,Nachingwea,Liwale na Ruangwa mnatakiwa kuchukua tahadhali kubwa kufuatia zaidi ya Magari 50 na watu wasiopugua 300 kushindwa kupita katika kijiji cha Chipite/Mkwera kufuatia eneo hilo kujaa maji yaliyotokana na Mvua zinazoendelea,

 Eneo hilo, ambalo lilitokea mafuriko makubwa mwaka 1990/1991, limeanza kujaa maji jana, hali ambayo leo imekuwa zaidi na kusababisha msongamano.
  Taarifa zaidi tutaendelea kuwapatia kadri hali inavyoendelea huku msaada wa haraka unahitajika ili kusaidia msongamano uliopo hapo ili kuepusha maafa mbalimbali

No comments:

Post a Comment

 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger