"Nimeandika barua Kwa Spika wa Bunge kutaka Waziri wa Nishati na Madini kutoa maelezo Bungeni kuhusu uamuzi wake wa kuwapa leseni kubwa ya kuchimba #Uranium huko wilayani Namtumbo. Mnamo tarehe 10 Agosti 2013 Waziri alitamka ndani ya Bunge "sisi tunajua zaidi ya anavyojua yeye, Leseni haijatolewa na haitatolewa mpaka Kampuni ya #MantraResources ilipe kodi".
 Kodi ya ongezeko la 
mtaji (capital gains tax) ya $189m kufuatia mauzo ya mradi wa #MkujuRiverProject 
kutoka kampuni ya Mantra kwenda kampuni ya AMRZ ya Urusi iligomewa kulipwa. #TRA 
wamepeleka shauri hilo mahakama ya kodi na mpaka sasa maamuzi hayajatolewa. Kwa 
mujibu wa mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2012, kabla ya Waziri mwenye dhamana ya 
madini kubariki mauzo ya kampuni, anapaswa kupata Kibali Cha kwamba kodi zote 
stahili zimelipwa. Kibali Kwa kampuni ya mantra kilitolewa bila kujali hitaji la 
kisheria na sasa kampuni hii imepewa leseni.
 Maamuzi haya ya Waziri 
wa Nishati na Madini yanalikosesha Taifa mapato ya zaidi ya tshs 300bn ambazo 
zingeweza kumaliza tatizo la nyumba za walimu nchi nzima na kulipia madai yote 
ya walimu. Fedha hizi zingeweza kujenga barabara ya lami kutoka Manyoni mpaka 
Itigi. Fedha zingeweza kukarabati reli ya Kati na kuirejesha katika ubora wa 
unaotakiwa. Kwa mujibu wa kanuni za Bunge nimetaka Waziri atoe maelezo bungeni 
na wabunge wajadili. Ni dhahiri kwamba serikali inayoongozwa na CCM imeamua 
kumaliza utajiri wote wa nchi na kuugawa Kwa wageni Kwa bei ya Che. Wananchi Ni 
lazima kusimama imara kukataa uporaji huu na maamuzi haya ya kiburi Cha kudharau 
Bunge yaliyoyafanywa na 
Serikali."
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment