Arnold Schwarzenegger anaidaiwa kuigiza kama adui kwenye ‘Avatar 2′. Kwa mujibu wa Latino-Review.com muigizaji huyo mkongwe amepata deal hiyo ya kuigiza ‘mtu mbaya’ kwenye filamu hiyo inayosubiriwa kwa hamu na inayoongozwa na James Cameron.
Avatar 2 itawakutanisha tena Schwarzenegger na Cameron ambao wamewahi kufanya kazi ‘Terminator’, ‘Terminator 2′ na ‘True Lies’.
Cameron alitangaza kuwa atakuwa akishoot filamu 3 za muendelezo wa ‘Avatar’ back to back kwa kuanzia mwakani lakini haijulikani kama Schwarzenegger atakuwepo kwenye zote.
Avatar 2 inatarajiwa kutoka December 2016, Avatar 3 December 2017 na Avatar 4 mwaka 2018