Search in This Blog

KUFURU: BABA YANGU MZAZI ALINIBAKA NA KUNIPA UJAUZITO INANIUMA SANA....


 Msichana ambaye amelalamikia kitendo alichokuwa akifanyiwa na baba yake mzazi wakati anapokuwa akishikwa na ugonjwa wa kuanguka na kupoteza fahamu kwa maana ya Kifafa.

 Kwa mujibu wa msichana huyu mkazi wa manispaa ya Tabora ambaye jina tunalihifadhi,amekuwa akifanyiwa tendo la kubakwa na Baba yake mzazi ambaye ni kiongozi wa dhehebu moja la dini pindi anapokuwa ameshikwa na tatizo la ugonjwa huo unaomkabili hatua ambayo alijikuta hata amepata ujauzito na kujifungua mtoto wa kiume.

Akisimulia mkasa huo msichana huyo alisema amekuwa akiumia moyo wake kila anapokumbuka kitendo hicho na wakati mwingine kila anapomuona mtoto anayedaiwa kuzaa na baba yake.

 

Pamoja na machungu anayoyapata amesema anakusudia kumfikisha Mahakamani Baba yake kwa kitendo alichomfanyia ambacho kwasasa kimekuwa kikimfedhehesha kutokana na kuzagaa kwa watu wengi.

 "Kaka yangu unamuona huyu mtoto ni Copywrite na baba yangu mi kwakweli inaniuma sana,kwanza siku niliyozinduka kutoka kwenye huo ugonjwa wangu nilimuona baba akiwa kifuani kwangu,nikamuuliza mbona unafanya hivyo?akanijibu we tulia tu tatizo nini."alisema msichana huyo huku akithibitisha kuwa hata mdogo wake wa kike alishuhudia mara kadhaa wakati akifanyiwa tendo hilo.

 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger