Jamaa mmoja si akakosea namba na akatuma Shs500,000/-kwa MPESA kwenda namba tofauti na aliyotaka? Hapo hapo akili ya haraka ikamjia akatuma SMS kwa hiyo namba kama ifuatayo.
MPENDWA
TUNATEGEMEA UMEPATA FEDHA ZETU. WEWE NI MMOJA ULIYEBAHATIKA
KUUNGANISHWA KATIKA KUNDI LETU TUKUFU LA FREEMASON. ILI KUKAMILISHA
MAKUBALIANO NDUGU YAKO WA KARIBU ATAFARIKI KATIKA MUDA WA MASAA MATATU
BAADA YA KUPOKEA FEDHA HIZO. MARA HILO LITAKAPOTOKEA FIKA UPESI KWENYE
NJIA PANDA YOYOTE ILIYOKARIBU NAWE, NA MTUMISHI WETU ATAKUFUATA NA GARI
JEUSI NAWE UTAKUJA KUNYWA DAMU YA KIAPO ILI UWE MWANACHAMA KAMILI.
KARIBU KWA FURAHA KUU.........
Dakika moja na nusu baadaye meseji ikarudi kwa jamaa ikisema
“D5RYE289 Imethibitishwa Umepokea Tsh510,000 kutoka kwa ………………………… Tarehe 10/10/13 saa 8:12 AM