Na Damas Makangale, Moblog kwa Msaada wa Mtandao
Msichana
Jacqui Beck (19) ni mtoto wa kike ambaye amezaliwa bila kiungo muhimu
cha Mwanamke (Uke) na hawezi kufanya ngono au kupata Watoto kutokana na
kukosekana sehemu yake ya Kike kama walivyo wanawake wote hapa duniani.
Beck
amesema kuwa alikwenda kwa madaktari kwa ajili ya uchunguzi na
wataalamu wamegundua baada ya vipimo kwamba msichana huo hana Ovary,
hana mfuko wa Uzazi wala Uke na hapati hedhi kila mwezi kama wanavyopata
Wanawake wenzake duniani.
Anasema
alipata mshtuko baada ya kuambiwa na madaktari kwamba hana Uke wala
sehemu ya siri haiwezi kufunguka na hiyo alikuwa na umri wa miaka 17 tu.
Beck
aliendelea kusema wakati akihojiwa na waandishi wa habari wa gazeti la
Daily Mail nchini Uingereza kwamba kwanza alikwenda kwa daktari wake
kuhusu maumivu ya nyuma ya mgongo na alikuwa hapati kabisa hedhi lakini
akitaka kujisaidia haja ndogo anaweza,” alisisitiza
Uchunguzi
wa madaktari umebaini kuwa hali yake si ya kawaida kwa sababu sehemu ya
Uke wake ipo kama giza au hamna kitu lakini haja ndogo inatoka lakini
hawezi kabisa kufanya mapenzi au kubeba ujauzito.
Madaktari
wanasema kwa Wanawake na kwa hali ya kawaida kabisa itaonekana nje –
lakini kwake ni kama hamna kitu bali ni sehemu tupu, msichana huyo Beck
anatoka kisiwa cha Wight yeye mwenyewe anasema anajisikia kama kituko
kwenye jamii.
Wataalamu
wanasema kwamba si jambo la kawaida kwa mwanamke (Abnormality) kwa
mtoto wa kike kuzaliwa hivyo lakini kati ya Wanawake 5000 wanaozaliwa
mmoja kupata tatizo hilo nchini Uingereza.
Wanawake
wanaosumbuliwa na hali kama hiyo kwa kawaida Ovary hawana lakini kupata
dalili ya kubalehe si kupata siku zao za kila mwezi au kupata ujauzito.