MASKINI! Msanii maarufu wa sinema za Kibongo, Michael Sangu ‘Mike’ amepata pigo la kuondokewa na dada yake, Salma Said na kujikuta akilia kama mtoto mdogo na kusababisha watu kuwa na kazi ya ziada kumbembeleza.
Mike Sangu akilia kwa uchungu baada ya kuondokewa na dada yake.
Mike alipatwa na pigo hilo wiki iliyopita baada ya dada yake huyo
kuugua kwa muda mfupi akisumbuliwa na maumivu ya titi moja lililokuwa
limevimba hali iliyosababisha kifo chake katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Dar.
Mike Sangu akilia kwa uchungu.
“Naumia sana, dada yangu alikuwa kila kitu kwangu kwani alikuwa
akinishauri mambo mbalimbali kuhusu maisha, ukweli ameniachia pengo
kubwa sana ila ndiyo mipango ya Mungu nitafanyaje,” alilalama Mike kwa
uchungu.
Ads not by this site
Mike Sangu (katikati) akilia kwa simanzi, kushoto ni mke wake Thea.
Mazishi ya dada huyo yalifanyika Ijumaa iliyopita katika Makaburi ya
Kinondoni, Dar na kuhudhuriwa na watu kibao wakiwemo waigizaji wa filamu
ambapo mkewe, Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ alikuwa na kibarua kizito
cha kumbembeleza Mike anyamaze.source:gpl