Mbunge wa Ukerewe, Salvatory Machemli.
DAR ES SALAAM. WABUNGE watatu na madiwani wawili wa Kanda ya Ziwa, wameshtakiwa mbele ya Baraza la Maadili ya Utumishi wa Umma kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za ukiukwaji wa maadili ya viongozi wa umma.

Viongozi hao pamoja na wanasheria watatu, akiwemo
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Sengerema Liveti Msangi na Mkurugenzi wa Jiji
la Arusha wanasomewa tuhuma zao hizo mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la
Maadili, Balozi, Jaji Mstaafu Hamis Msumi na wajumbe wawili wa baraza
hilo, Hilda Gondwe na Celina Wambura.
Akizungumza na waandishi wa habari Nov 15 mwaka huu, Kaimu
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Tixon Nzunda
alisema baraza hilo linaendelea kusikiliza kesi hizo mkoani Tabora,
ambapo wananchi wanaruhusiwa kusikiliza kesi hizo huku Sekretarieti hiyo
ndiyo mlalamikaji.
“Kama nilivyosema ni baraza la wazi, ni viongozi mbalimbali walioshtakiwa huko, lakini kwa kuwa mimi simo miongoni mwa wanaoendesha kesi hizo sipo tayari kuwatajia,” alisema Nzunda.
“Kama nilivyosema ni baraza la wazi, ni viongozi mbalimbali walioshtakiwa huko, lakini kwa kuwa mimi simo miongoni mwa wanaoendesha kesi hizo sipo tayari kuwatajia,” alisema Nzunda.
Hata hivyo, habari za uhakika kutoka katika vyanzo
vyetu vya habari, wabunge hao wametajwa kuwa ni Lameck Airo (Rorya),
Salvatory Machemli (Ukerewe) na Suleiman Suleiman (Kishapu).
Madiwani wanaoshtakiwa kwenye baraza hilo ni
Mathias Bisoma (Kata ya Kanazi, Kagera), Meya wa Jiji la Mwanza Henry
Matata ambaye ni Diwani wa Kata ya Kitangiri.
Viogozi wengine walioshtakiwa na Sekretarieti ya
Maadili katika Baraza hilo ni Mwandishi Mkuu wa Sheria, Casmir Sumba
Kyuki na Mkurugenzi Msaidizi Uandishi wa Sheria, Sarah Kinyamfura
Barahomoka.
Miongoni mwa mashtaka yanayowakabili viongozi hao
ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka, huku wengine wakidaiwa
kushindwa kuwasilisha matamko ya rasilimali zao.
Awali, Nzunda alifafanua kuwa kesi hizo
zitasikilizwa kwa wiki mbili, ambapo mashahidi ni wananchi. Baraza hilo
ni taasisi huru inafanya kazi zake kwa mara ya kwanza baada ya
kuchanguliwa na kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete, Julai mwaka huu. MWANANCHI