Stori: Global Publishers
Dalili za kifo zipo nje nje,
zinajidhihirisha kwa ukaribu zaidi katika maisha ya Mbunge wa Urambo
Magharibi (CCM), Profesa Juma Athuman Kapuya, sababu kuu ikiwa zigo la
tuhuma za kumbaka na kumwambukiza Ukimwi mwanafunzi.
Siyo Kapuya tu, hata mwanafunzi anayedai
kubakwa na waziri huyo wa zamani, naye maisha yake siyo salama, kwa
hiyo rai imetolewa kwa wote wawili kupewa ulinzi stahiki.
Tuhuma kuu ni Kapuya kuripotiwa na
gazeti pamoja na mitandao kadhaa ya intaneti, akidaiwa kumbaka
mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 16 (jina tunalihifadhi),
anayesoma Shule ya Sekondari Turiani, Magomeni, Dar es Salaam.
Mwanafunzi huyo amekuwa akinukuliwa na
vyombo vya habari akisema kuwa alibakwa mara mbili na Kapuya kisha
kuambukizwa Ukimwi wakati alipokwenda kumuomba msaada wa ada ya shule
kwa sababu yeye ni yatima.
KAPUYA NA KIFO
Kapuya, aliye kiongozi mwandamizi wa
Tanzania, akiongoza wizara mbalimbali kama vile Elimu, Kazi, Vijana na
Ajira, Habari, Utamaduni na Michezo, Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na
kadhalika, maisha yake yapo hatarini kwa sababu zifuatazo;
MOSI; Wananchi waliozungumza na Risasi
Jumamosi, wamesema kuwa hatari ya kwanza ni SMS ambayo inadaiwa Kapuya
aliituma kwa mwanafunzi huyo akimtishia kumuua.
“Kapuya ni kiongozi mwenye heshima kubwa
nchini, kukumbwa na tuhuma za kutishia kuua siyo dogo,” alisema Phabian
Tarimo ambaye alidai ni jirani wa mwanafunzi huyo na kuongeza:
“Inawezekana kujiepusha na aibu hiyo ya tuhuma za ubakaji au kutishia kuua, akaamua kujiua.”
PILI; Kingine ambacho kinaashiria hatari
kwa maisha ya Kapuya ni SMS ya kutishia kujiua ambayo inadaiwa kiongozi
huyo alimtumia denti mlalamikaji.
Vyanzo vyetu vinasema, SMS hiyo kutoka
kwa Kapuya inasomeka: “Nimewakosea sana, acha nife mie nakunywa sumu
nijiue, na nyie mje mnizike.”
Mchangia maoni mmoja wa mtandaoni,
Lubelo Issa, alisema: “Kapuya kutamka kujiua siyo jambo dogo, naamini
anamaanisha, inabidi familia yake na marafiki zake wawe karibu naye.
“Ikiwezekana hata polisi wawe macho,
maana hilo ni kosa la jinai. Kwa mtu mkubwa kama Kapuya kupewa tuhuma
nzito kama hizo, ni rahisi kumkatisha tamaa. Ni rahisi kuuona mwisho
wake wa kisiasa.
“Hali yake mbele ya familia yake ipoje? Hayo mambo ni mzigo ambao unaweza kumpeleka mbali hadi kufikia hatua ya kujiua.”
DENTI NA KIFO
MOSI; SMS ambayo amedai kutumiwa na
Kapuya ni hatari ya kwanza na katika hilo, imeshauriwa na wananchi
kwamba denti huyo alindwe usiku na mchana.
“Kapuya amechafuka sana na ikiwa ni
kweli zile SMS zimetumwa na yeye, basi yule mtoto achungwe na alindwe
kikamilifu. Kapuya amejenga heshima yake kwa miaka mingi, hawezi
kukubali kuchafuliwa kienyeji.
“Inawezekana Kapuya akawa na moyo wa
subira pamoja na huruma lakini wapo wapambe ambao wanaweza kuchukua
hatua ya kumuua yule mtoto kwa sababu amemchafua bosi wao.”
PILI; Sura ya pili ambayo imeangaliwa
kuhusu hatari ya maisha ya denti huyo ni kwamba Kapuya anao maadui wa
kisiasa ambao wanaweza kutumia mgogoro huo kujifaidisha.
Laura Kamugisha aliandika kwenye ukurasa
wake wa Facebook: “Kuna sayansi moja hapa, adui wa Kapuya anaweza
kumuwinda huyo mwanafunzi na kumuua ili kuzidi kumuweka Kapuya matatani.
“Leo ikitokea huyo mwanafunzi ameuawa,
kila mmoja fikra zake zitaelekezwa kwa Kapuya. Kwa kweli huyu mtoto yupo
hatarini, inawezekana Kapuya akampuuza lakini maadui zake wakamuua ili
kumkomoa. Mwanafunzi akiuawa, Kapuya atapelekwa mahabusu na baadaye
mahakamani.”
SHAHIDI MUHIMU AZUNGUMZA NA RISASI JUMAMOSI
Mrembo (jina tunalo) ambaye ni rafiki wa
denti anayedai kubakwa, alisema kuwa ameshangaa kusikia suala hilo
limefika kwenye vyombo vya habari kwa sababu huko nyuma yeye
alishalisimamia na mambo yakaisha.
“Sijui kuhusu kubakwa, ila … (anataja
jina la denti) aliniambia madai yake, nikampeleka kwa mheshimiwa, kusema
kweli nilimbana mheshimiwa na fedha zilitoka. Mimi mwenyewe nilipata
mgao,” alisema mrembo huyo.
Akaongeza: “Ninavyojua walikubaliana,
siyo kubakwa. Na mimi nilimsaidia kumbana mheshimiwa ili ampe pesa.
Alikuwa anahitaji pesa ya kwenda kulipa ada shuleni, pesa alipewa.
“Nilianza kuwa mbali naye baada ya kuona
amekuwa karibu na wanaharakati. Kuanzia hapo hakunishirikisha kitu,
japo tunawasiliana. Hata leo nimeongea naye, ameniambia yupo… (anataja
eneo moja, nje ya Dar).
“Kingine ni kwamba wakati namsaidia ishu
yake na mheshimiwa alikuwa anasoma Mugabe Sekondari, sijui Turiani
alihamia lini. Na kuhusu Ukimwi mimi sijui hilo, ila natambua kwamba
yule mwanafunzi anatumia dawa.
“Hapa lazima niwe mkweli, siwezi kuthibitisha kama kweli ni Ukimwi na kama ni kweli aliyemwambukiza simjui,” alisema.
KAPUYA VIPI?
Juzi, mwandishi wetu alijitahidi kwa
kila namna kumpata Kapuya kupitia simu zake tatu za mkononi, mbili za
Airtel na moja ya Vodacom lakini hakupatikana.
Mbili hazikuwa zikipatikana lakini moja
ilikuwa ikiita bila kupokelewa, ingawa wakati mwingine ilipopigwa
ilionesha mwenye simu alikuwa akizungumza, hivyo kuonesha hakutaka
kuwasiliana na mwandishi wetu.
Pamoja na kutumiwa SMS inayomuuliza
kuhusu tuhuma hizo, bado Kapuya ambaye kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, hakutoa ushirikiano.
Kuhusu mwanafunzi huyo, Risasi Jumamosi
linatambua yupo mafichoni na ahadi yetu ni kuendelea kutoa taarifa zaidi
kuhusu tukio hilo kupitia magazeti pendwa ya Global Publishers Ltd.
-Global Publishers