Search in This Blog

HOFU YA MASTAA KUTABIRIWA VIFO YAWAFANYA WAKOSE AMANI


HOFU ya kifo imetawala kwa mastaa Bongo ikiwa ni siku chache baada ya gazeti hili toleo la Jumamosi iliyopita kutoka na habari ya utabiri wa Hussein Yahaya, ikieleza kuwa mwaka huu vifo zaidi vitaendelea kwa wasanii wa filamu, muziki, waandishi wa habari, viongozi wa dini na wanasiasa.

Aunt Ezekiel.
Risasi Mchanganyiko limepata kuzungumza na baadhi ya wasanii wa sanaa mbalimbali Bongo na kueleza maoni yao kuhusiana na utabiri huo. Wa kwanza kuzungumza alikuwa ni Single Mtambalike ‘Richie’ aliye msanii wa filamu ambaye alisema:
“Namwamini Mungu kwa asilimia zote, hata kama kitatokea kifo mbele yetu nina imani kitakuwa na sababu kama ugonjwa na kadhalika, siyo ghafla."
SHAMSA FORD
"Unajua ibada ndiyo kitu cha kwanza kutuokoa, mimi natoa rai kwa wenzangu wakumbuke kuomba kila mtu kwa imani yake tutashinda tu."

AUNT EZEKIEL
"Haya yanayotokea inabidi tujifunze na yaliyopita, mimi kwangu naona kama changamoto nyingine. Naahidi kumtukuza Mungu ili niepukane na balaa hili."

BEN POL
Huyu ni mkali wa R&B, yeye alisema: “Tukazane kumuomba Mungu kwa njia yoyote ile tutashinda hili jaribu."

SNURA MUSHI
Aliibukia kwenye filamu lakini sasa yupo pia kwenye muziki, akiwa ametambulishwa na kibao chake cha Majanga. Yeye alisema: “Mwaka uliopita  ulikuwa wa majanga sana, nawashauri wenzangu tukimbilie sala maana ndiyo kimbilio letu la mwisho."
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger