Mgahawa wa kwanza maalum kwaajili ya mbwa na paka uitwao ‘Pets Deli’ umefunguliwa huko Berlin, Ujerumani.
Kati ya vyakula vinavyopatikana katika menu ya mgahawa huo ni pamoja na beef, bata mzinga, cupcakes, wali, viazi bila kusahahu nyama ya Kangaroo.
Mgahawa huo uliofunguliwa katika kipindi cha Christmas mwaka jana 2013, vyakula vya wanyama hao vinauzwa kuanzia €3 hadi €6 (6500-13000Tsh).
Katika mgahawa huo kuna sehemu imetengwa kwaajili ya wamiliki wa wanyama hao kupata kahawa wakisubiri mbwa na paka wao wapatiwe huduma.
Mmiliki wa mgahawa huo David Spanier (31) alisema alipata wazo baada ya kugundua rafiki yake hua anashindwa kutumia vyakula vya supermarket kwaajili ya wanyama kutokana na kuwa junk food.
Spiner aliongeza kuwa nyama inayoandaliwa ina ubora ambao inaweza hata kuliwa na binadamu bila tatizo.