Tukio hilo lilitokea siku ya Ijumaa
usiku maeneo ya Carribean Sinza jijini Dar es Salaam ambapo alivamiwa
na watu hao wasiojulikana kwa nia ya kumfanyia uhalifu wa kumpora vitu
vyake.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii
Mez alidai kuwa alikuwa akitokea kwa msanii mwenzake ambaye ni rafiki
yake wa muda mrefu Noura ndipo mkasa huo ulipomfika.
Alidai kuwa watu hao walikuwa wawili
walimvamia akiwa anasubiri usafiri wa kurudi kwake na kumuibia walety
yake ambayo ilikuwa na fedha ingawa hakutaka kuweka wazi kiasi cha
fedha walichochukua.
Alisema kuwa alijitahidi kupambana nao
hali ambayo haikuzaa matunda na ndipo alipoweza kumjeruhi usoni
majeraha makubwa yanayosababisha ashindwe kutembea.
"Walinivamia watu wawili, ambao
sikuweza kuwafahamu na mbaya zaidi najeruhiwa na watu hao bila ya
kupata msaada wowote ule wamefanikiwa kuniibia ingawa simu walishindwa
kuichukua" alisema Mez B.