Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe amefungua mashtaka kwa madai kwamba anatishiwa maisha kufuatia hekaya inayoitwa "Ripoti ya siri ya Zitto Kabwe".
Mbunge huyo amepost picha yake akiwa
makao makuu ya polisi Dar es Salaam na kuandika maelezo yafuatyo kupitia
ukurasa wake wa facebook:
"Nimetoka makao makuu ya polisi, upelelezi, kuandika statement kuhusu vitisho dhidi yangu kufuatia hekaya inayoitwa "Ripoti ya Siri ya Zitto Kabwe". Chanzo cha hekaya sasa kinabadilishwa kutoka makao makuu ya CHADEMA na kuwa ni usalama wa Taifa au CCM.

Wahusika waendelee kuhamisha chanzo
lakini wajue watasakwa na kukamatwa na kuburuzwa mahakamani.
Nimewashitaki kwa kunitishia maisha. Ninawashitaki kwa kunichafua kwa
tuhuma za uongo.
Ninafanya haya kwa lengo la kuhakikisha kuwa siasa za kuzushiana na kusambaza uongo zinakuwa na gharama kubwa.