MSANII wa filamu Bongo, Michael Sangu ‘Mike’ amepata pigo la kufiwa
na dada yake, Salma Said aliyefariki juzi katika hospitali ya Taifa
Muhimbili na kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam.
Ibada ya mazishi na zoezi la kuaga mwili wa marehemu
imefanyika katika kanisa la Wasabato, Mburahati na baadaye mwili kuzikwa
katika makaburi ya Kinondoni.
-GPL