Mwanamuziki
kwenye muziki wa kizazi kipya Bob Junior hivi karibuni amefunguka na
kuweka wazi sababu zilizomfanya aamue kuachana na mke wake.
Katika
mahojiano niliyofanya naye kwenye kipindi cha The Takeover, TBC fm,
mnamo siku ya Jumanne, Bob Junior alifunguka na kueleza mambo mengi huku
akikiri kwamba ni kweli kuwa amemuacha mke wake, "mwanamke anataka kuwa
kama mume ndani ya nyumba, amefikia hadi hatua haongei na mama yangu
mzazi" alisema Bob Junior.
Nilimuuliza
pia juu ya idadi ya taraka alizompa, " mimi nimempa taraka tatu maana
nimemaliza kabisa" alisema mkali huyo ambaye kwa sasa anatamba na ngoma
yake mpya iitwayo Bashasha aliyomshirikisha Vanessa Mdee.