Search in This Blog

PENNY BAADA YA KUTEMWA NA DIAMOND MAMBO YAZIDI KUMUENDEA KOMBO, ONA HAPA MWENYEWE

KATIKA staili ya aina yake ya kuuaga mwaka na kuukaribisha 2014, mtangazaji Peniela Mungilwa ‘Penny’, ambaye ni zilipendwa wa Nasib Abdul ‘Diamond’ alipewa zawadi ikiwemo keki yenye maandishi ya kumsuta.
 
Peniela Mungilwa ‘Penny’.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Jumatano hii nyumbani kwake Mwananyamala Mwinjuma alikohamia hivi karibuni, baada ya watu wanaosadikika kuwa ni wadau wa Wema Sepetu, kufika hapo wakiwa na ‘mzigo’ huo uliojumuisha pia kadi, shampeni na maua.
Mmoja wa wapangaji wa nyumba anayoishi Penny, aliliambia gazeti hili kuwa msafara wa magari matatu ulifika hapo na kugonga mlango wakimuulizia mtangazaji huyo wa kituo cha televisheni cha Channel Ten.
“Walivyofika sisi tulijua labda leo ni bethidei ya Penny, maana tuliwaona wakiwa na maua, keki, shampeni na kadi, walipomuulizia tukawaambia ametoka, wakaacha mzigo huo wakisema apewe atakaporudi,” alisema shuhuda huyo.
 
Juu ya Keki iliyopelekwa kwa mtangazaji huyo kulikuwa na maandishi yaliyomsuta na kumtaka kuachana na tabia ya kuchukua mabwana wa rafiki zake pamoja na dada zake, hali inayoonyesha kuwa waliompelekea ujumbe huo ni wabaya wake.
Juhudi za kumtafuta Penny kuzungumzia tukio hilo hazikuweza kuzaa matunda hadi gazeti hili linakwenda mtamboni.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger