Search in This Blog

UKWELI KUHUSU SAYANSI YA KIAFRIKA AKA UCHAWI

Sayansi maana yake ni maarifa . Tunapo zungumzia dhana ya sayansi ya kiafrika , tunakuwa tunamaanisha matumizi ya maarifa ya kiafrika katika kukabiliana na mazingira ya mwanadamu pamoja na changamoto mbalimbali zinazo mkabili .

Tafiti mbalimbali za ki akiolojia na ki-anthropolojia zinaonyesha kuwa sayansi ya kiafrika imekuwapo kwa takribani miaka bilioni mbili sasa, hii ikiwa na maana kuwa sayansi ama ustaarabu wa kiafrika ndio ustaarabu mkongwe kupita ustaarabu mwingine wowote ule katika sayari ya dunia.

Hata ustaarabu wa jamii mbalimbali duniani kama vile waajemi, wayunani (Ugiriki ya kale ), wamisri, wasumeri ( Mesopotamia/babiloni ) ya kale nakadhalika, unatokana na ustaarabu ambao msingi wake ni sayansi ya kiafrika.

• Sayansi ya kiafrika imethibitika kumsaidia mwanadamu katika kukabiliana na mazingira yake kwa zaidi ya asilimia tisini na tisa (99%).

• Kwa bahati mbaya sana, sayansi ya kiafrika imepewa jina baya kwa kuitwa uchawi na kupigwa vita mbaya tangu mamia ya miaka iliyopita, lengo kuu likiwa ni kumuondolea mwanadamu uwezo wa kiungu ulio wekwa ndani yake wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazo mkabili katika maisha yake ya kila siku.

• Hata hivyo watu hawa walio mstari wa mbele katika kuipiga vita sayansi ya kiafrika, bado wanaendelea kuitumia sayansi ya kiafrika katika maisha yao ya kila siku japo kwa usiri mkubwa sana, ilihali wakati huo huo wakiendelea kuipiga vita sayansi hii. Watu hawa wanataka maarifa haya yawe ni kwa watu wachache.

• “ The Choosen Few “ huku mamilioni ya walio baki wakiendelea kuishi katika giza bila kujua kitu chochote kile kinacho endelea kwenye maisha yao. Hali hii imewafanya waendelee kuitawala dunia kwa muda mrefu sana kwa kutumia nyenzo mbalimbali za ku-control fikra za wanadamu.

Hofu kuu ya watu hawa ni kwamba, endapo kila mwanadamu ataifahamu vyema misingi ya sayansi ya kiafrika, itakuwa vigumu sana kwa wao kumtawala kwa sababu kila mtu atakuwa na uwezo wa kuyatawala mazingira yake na kukabiliana na changamoto za aina yoyote ile zinazo yakabili maisha ya kila siku ya mwanadamu…

• Sayansi ya kiafrika humjengea mwanadamu uwezo wa kuwa na mamlaka juu ya vitu vyote vilivyopo hapa duniani, vinavyo onekana na visivyo onekana. Humpa uwezo wa kuvitiisha vitu vyote vilivyo na uhai na visivyo na uhai.. Kwa ufupi inamfanya kuwa na umoja na Mungu.

• Miongoni mwa mambo ya kawaida kabisa anayo fundishwa mwanadamu katika sayansi ya kiafrika ni pamoja na :

• Somo la AKILI-UMEME-SAUTI ama MIND-ELECTRICITY-SOUND . Elimu hii humpa mwanadamu uwezo wa kuwa- control wanadamu wenzake kifikra, uwezo wa kuwatawala majini na viumbe wasio onekana na macho ya nyama, uwezo wa kuumba vitu, mambo na hali za aina mbalimbali kwa kutumia maneno, uwezo wa kupeleka heri au shari kwa wanadamu, wanyama, mimea na roho, uwezo wa kuvitiisha viumbe vyote vya nchi kavu,uwezo wa kutumia nguvu ya akili katika kufanya mambo mbalimbali nakadhalika.

• Somo la UMEME & HEWA au ELECTRICITY & AIR. Elimu hii humpa mwanadamu uwezo wa kupaa angani, uwezo wa kuitiisha anga na viumbe vyote vya angani, uwezo wa kuwasiliana na kuvi control viumbe vinavyo ishi kwenye upepo, uwezo wa kupeleka ujumbe kutoka sehemu moja ya dunia kwenda sehemu nyingine yoyote ile, uwezo wa kusafiri angani nakadhalika.

• Somo la NECROMANCIA ama NEGROMANCIA ambalo humpa mwanadamu uwezo wa kuwasiliana na kuzungumza na roho za watu walio kwisha kufa.

• Uwezo wa kuwasiliana na viumbe vya mtoni, ziwani na baharini
• Mamlaka ya kuvitiisha viumbe vyote vya duniani, vya nchi
kavu, baharini, na angani, vinavyo onekana na visivyo onekana.
• Uwezo wa kuona vitu visivyo onekana na wanadamu
• Uwezo wa kusikia sauti zisizo sikiwa na wanadamu.
• Uwezo wa kufanya mambo katika namna ya kiungu.
o Hayo ni moja kati ya maaarifa machache yanayo patikana katika sayansi ya kiafrika.

• Kwa ufupi, sayansi ya kiafrika inampa mwanadamu mamlaka kamili ya kuwa kitu kimoja na Mungu. Mfalme Suleiman ni miongoni mwa wanadamu walio pata bahati ya kupewa maarifa haya, habari zake nadhani wengi wetu tuna zifahamu.

• Endapo wanadamu watazingatia misingi ya sayansi ya kiafrika, basi wataweza kuyatawaka mazingira yao pamoja na changamoto mbalimbali zinazo wakabili kwa kiwango kikubwa sana.

• MUNGU NI NANI KWA MTAZAMO WETU?
• Kwetu sisi MWENYEZI MUNGU ni NGUVU KUU YA UHAI ( THE MOST GREATEST FORCE OF LIFE ). Nguvu Ya Uhai ni nini ? Nguvu ya uhai ni roho ama nishati inayo vifanya viumbe viishi na/ama viwepo au ni roho ama nishati inayo weka uhai kwenye viumbe vyote vinavyo onekana na visivyo onekana. Hivyo basi kwetu sisi MWENYEZI MUNGU ndio NGUVU KUU YA UHAI, kwa maana yeye ndio chanzo cha uhai wa kila kiumbe cha hapa duniani, kinacho onekana na kisicho onekana.

• Wakati mwingine huwa tunamtaja Mungu kama MOVENS IMMOBILE yaani UNMOVED MOVER.

• UHUSIANO KATI YA MUNGU NA MWANADAMU.
• Sisi tuna amini kuwa MUNGU NA MWANADAMU ni kitu kimoja.

Mwanadamu anatoka kwa MWENYEZI MUNGU. Kama nilivyo eleza hapo awali, Mwenyezi Mungu ndio NGUVU KUU YA UHAI, ndio CHANZO KIKUU CHA UHAI, hivyo basi kila kiumbe chenye uhai kinatoka kwenye chanzo cha uhai, nguvu inayo mfanya mwanadamu aishi, inatoka kwa Mungu, nguvu hiyo ni Mungu mwenyewe, kwa maana nyingine mwanadamu ni muungu mdogo, Mungu anajidhihirisha kupitia huyu mwanadamu. Kwa lugha nyingine ni kwamba, wanadamu ni vidhihirisho vya pembeni vya CHANZO KIKUU CHA UHAI.

Vidhihirisho hivi, vinapotambua nguvu iliyopo ndani yake na kuanza kuitumia vyema, NGUVU KUU YA UHAI ambayo ndio chanzo kikuu cha uhai, hujidhihirisha pamoja navyo, inapofikia hatua hii, vidhihirisho hivyo huwa kitu kimoja na kidhihirisho kikuu na hufanya mambo yake katika mfano wa CHANZO KIKUU CHA UHAI.

YESU alilitambua hili ndio maana ali fanikiwa ku atain eternity akiwa duniani, mara nyingi alikuwa akisema “ MIMI NA BABA TU KITU KIMOJA “. Hapa alimaanisha kuwa yeye na Mungu ni kitu kimoja, sio katika form ( muundo) bali katika consciousness. Wayahudi hawakulitambua hili ndio maana walidhani anakufuru.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger