NI
kipindi cha kuukaribisha mwaka mpya 2014 na kuuaga 2013. Katika kipindi
hiki ni desturi yetu kuwanunulia tuwapendao zawadi na pengine hata
kujinunulia wenyewe kama ishara ya kutakiana maisha mema na yenye afya
tele.
Kuna zawadi nyingi za kumnunulia umpendae lakini pengine inayoweza
kuwa na thamani kubwa na yenye mvuto kwa kipindi hiki ni lishetiba au
kwa jina lingine ‘food supplement’ kwa sababu utakuwa umeboresha afya
zao baada ya kutumia zawadi hiyo.
Lishetiba zilianza kutengenezwa miaka takribani 50 iliyopita. Hii
ilitokana na wanasayansi kubaini kuwa lishe duni ndiyo chanzo cha
magonjwa mengi. Wengi waliotumia lishetiba walipona maradhi ya aina
mbalimbali.
Mwaka 1994 Baraza la Congress la Marekani liliamua kuweka sheria ya
lishetiba (isipokuwa tumbaku na mazao yake) kuwa zitengenezwe, ziuzwe na
zitumike chini ya mamlaka na sheria za vyakula.
Pia watengenezaji wa lishetiba walishurutishwa kuweka lebo katika bidhaa zao ikionyesha wazi kuwa si dawa ila ni chakula tu.
Kwa kuwa lishetiba hizo zilizalishwa zaidi ya aina elfu 50, sheria
ilitoa maelekezo kuwa lishetiba zote zitumiwe na walaji kupitia mdomoni
tu na siyo vinginevyo, awali zilikuwepo mpaka sindano na dripu kama
hospitali.
Kadiri dunia inavyoongezeka watu ndivyo fursa ya kupata mlo sahihi
inakuwa ngumu na hivyo suala la kujazia upungufu huo kwa kula lishetiba
linakuwa ni jambo la lazima.
Kuna aina nyingi za lishetiba, mfano zipo za kuimarisha kinga ya
mwili (antioxidant) ambazo zina vitamin C na E, kuna magome ya
mkaratusi, juisi ya zabibu ambayo hutoa ahueni kwa wagonjwa wa saratani
na wenye maradhi ya moyo, pia imethibitika kuufukuza uzee kwa kufuta
makovu na makunyanzi ya uzee huku ikiiacha ngozi iking’ara zaidi na mzee
akaonekana kama kijana.
Aidha, zipo lishetiba za ubongo ambazo zimethibitika kuuchachua
ubongo wa mlaji na kuimarisha kumbukumbu zake hivyo kuondoa tatizo la
usahaulifu kwa watu wazima na hata wanafunzi. Pia zipo za kuimarisha na
kuondoa matatizo kwenye mfumo wa nguvu za uzazi.
Tibalishe zipo za kila aina na kwa kila tatizo, ila hatuwezi kuzitaja
zote leo hapa. Tanzania bado ipo nyuma sana katika matumizi ya
lishetiba ulinganisha na nchi zingine duniani ambazo zimeweka utaratibu
kwa kuuza ‘kila kona’ kuanzia hospitali, maduka ya dawa baridi hadi
hotelini na hivyo kufanya upatikanaji wake kuwa rahisi.
Ni ukweli uliowazi kuwa siyo rahisi kupata mlo kamili wenye
virutubisho vyote wakati wote, hivyo ni vyema ukajazia upungufu huo kwa
kula lishetiba ukiwa na wasaa huo. Sisi kama chombo cha habari
tunakuahidi ushirikiano wa dhati katika hili, hivyo usisite kuwasailiana
nasi kwa msaada zaidi.