Fataki hizo zilidumu kwa dakika sita kuanzia saa 6 kamili usiku wa 01/01/2014.
Jengo la Burj Khalifa Dubai wakati wa mchana
Waandaaji wa fataki hizo walilenga kuvunja rekodi iliyowekwa mwaka 2012 katika Golden Jubilee Anniversary ya Kuwait.
Jumla ya computer 100 zilitumika kuleta muonekano wa fataki hizo za Dubai zilizoambatana na muziki uliotengenezwa maalum kwaajili ya shughuli hiyo (choreographed musical soundtrack).
Rais wa Guinness World Records Alistair Richards aliyesafiri kutoka Uingereza hadi Dubai maalum kwaajili ya kushuhudia fataki hizo wakati wa kuupokea mwaka mpya alisema, “The scale of this record attempt is truly impressive and will ensure all eyes are on Dubai”.
Tazama video ya fataki hizo