Search in This Blog

STEVE NYERERE AWAFUNGUKIA WANAOMZUSHIA KUWA YEYE NI SHOGA


Mwenyekiti wa bongo movie Unity, Steve Nyerere amechukizwa na watu wanaotumia mitandao vibaya na kwa kumzushia kuwa ni shoga.
Steve Nyerere kupitia akaunti yake ya facebook ameandika: Napenda kuchukua fursa hii kuongea machache na kama mtaboa mtu naomba samahani najua binadamu tumezaliwa tofauti sana kuna wale wanaogopa zambi na kunawale wanopenda zambi mimi daima nasema izo ni changamoto tuuu ok nimepata taarifa umu umu kwenye mitandao yetu ya kijamiii hususani huuu kwamba kuna binti anaitwa zainab ananichafua na kuniandika mambo ambayo ayana tija kwangu. 
Nazani ata kwake kwamba mimi shoga anauhakika hahahahaha nimecheka sana kupata izi taarifa nataka kuwapa taarifa ndugu zangu kuna msemo unasema mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe na mkanya mara moja aache mara moja kwani naimani anapoteza muda tu habari hizo si zakweli kabisa ila namtakia laheli kwahili jambo analonitendea mimi nasema namwachia mola akumbuke nafamily mke na watoto mama dada zangu kiukweli najisikia vibaya sana mi nasema asante”.
Baada ya kuandika kauli hiyo, Steve Nyerere ameuambia mtandao wa bongo5 kuwa kuna watu wameamua kumchufua baada ya kujionyesha wazi kwenye siasa.

Watu wananitumia meseji mbaya, eti mimi nimetumwa na viongozi, mara sijui mimi ni shoga, jamani hakuna mambo kama hayo, nawataka watanzania wajue hayo ni mambo za uzushi, sijui ata yametoka wapi Alisema Steve Nyerere

WATU 5 PAPO HAPO BAADA YA LORI KUGONGA KILABU CHA POMBE IRINGA

Maiti nne za marehemu ambao walifariki papo hapo baada ya Lori hilo kugonga kilabu hicho ikiwa imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa ya Iringa.
unnamed
Lori la Mizigo likiwa limepaki katikati ya kilabu hicho cha pombe ambacho kilisambalatishwa chote na chini ni mabaki ya kilabu hicho.
unnamed (9)
Mashuhuda wakiwa wanashuhudia ajali hiyo baada ya kutokea .
unnamed (11)
 Baadhi ya wananchi wa Eneo la Isimila wakiwa wameongezeka kushuhudia ajali hiyo mbaya iliyouwa wata watano papo hapo.
unnamed (12)
 Hivi ndivyo Lori hilo la Mizigo lilivyo umia vibaya baada ya kugonga kilabu hicho na kukisambalatisha usiku wa kuamkia jana na kusababisha vifo vya watu watano papo hapo.
unnamed (13)
Baadhi ya Ndugu wa Marehemu wakipata taarifa za Ajali hiyo katika eneo la tukio Isimila.
unnamed (14)
Ndugu wa Marehemu wakiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa kwa ajili ya kutambua miili ya marehemu hao.(Picha zote na Iringa Yetu Blog).
unnamed (15)

HII NDIO SHULE YA KATA ILIYOSHIKA NAFASI YA 3 KITAIFA

Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kisirimi wilayani Arumeru, Arusha, Emmanuel Kisongo amesema kufanya vizuri kwa shule yake ni kuthibitisha shule za kata zinaweza kuwa bora nchini.

Kismiri (pichani) imeshika nafasi ya tatu kati ya shule 10 bora nchini mwaka huu, kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa jana na Baraza la Mitihani Tanzania (Necta).

Akizungumza na Mwananchi jana, Mwalimu Kisongo alisema mwaka huu wanafunzi wa shule yake wamefanya mtihani wa kidato cha sita kwa mara ya saba na shule imefanikiwa kushika nafasi ya tatu kitaifa kwa mara ya kwanza.

Nimefurahi tumeingia kwenye shule 10 bora nchini mara tano na safari hii tumeshika nafasi ya tatu. Ni wazi shule za kata zinaweza, tofauti na fikra za wengi kuwa shule zipo chini kielimu,” alisema.

Kisongo alisema mwaka jana walishika nafasi ya tano, kitaifa na mwaka juzi, walishika nafasi ya tatu kama mwaka huu.

Siri ya mafanikio yetu ni ufundishaji mzuri na ushirikiano mzuri wa walimu, wanafunzi na wazazi kwa lengo kubwa la kuthibitisha kuwa walioanzisha shule ya kata hawakufanya makosa,” alisema.

Alisema shule yake, ambayo ina jumla ya walimu 32 kati yao 12 wanafundisha kidato cha tano na sita, inafuata michepuo ya sayansi na sanaa (art) na mwaka huu wanafunzi 52 walifanya mtihani.

“Tunajivunia mafanikio haya na malengo yetu kuifanya shule hii kuwa bora nchini kwani ipo katika mazingira tulivu na wanafunzi wa dini zote tunawajenga kuwa na hofu ya Mungu,” alisema.

Alisema kwa sasa wanafunzi wa shule hiyo, wanajitambua na wanaheshimu masomo yao. Hawana muda wa migogoro na shule, jambo ambalo linawapa muda mzuri kusoma.

Shule 10 bora 2013 zaporomoka
Dar es Salaam. Shule za sekondari zilizokuwa kwenye orodha ya Kumi Bora ya matokeo ya kidato cha sita mwaka jana zimeporomoka, huku shule isiyo maarufu ya Igowole, mkoa wa Iringa ikichomoza kutoka nafasi ya nane hadi ya kwanza mwaka huu.

Mazingira ya Shule ya Sekondari ya Igowole iliyopo Wilaya ya Mufindi ni ya kawaida sana, huku kwa muda mwingi wa msimu wanafunzi wakipigwa na baridi kali katika eneo lilipo shule hiyo iliyozungukwa na miti mikubwa.

Katika matokeo ya kidato cha sita mwaka jana, Necta ilipanga shule 10 bora kulingana na idadi ya watahiniwa juu ya 30 na chini ya 30, lakini mwaka huu imeziweka kundi moja, kwa mujibu wa kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles E. Msonde.

Mwaka jana, kati ya shule 10 zilizokuwa na watahiniwa zaidi ya 30, ni shule nne pekee zimeendelea kuwamo katika kundi la shule 10 bora kitaifa mwaka huu licha ya mabadiliko hayo. Shule hizo ni Marian Girls (Pwani) imekuwa ya sita mwaka huu wakati ilishika nafasi ya kwanza 2013. Shule ya Feza Boys (Dar es Salaam) imeshika nafasi ya pili mwaka huu wakati mwaka jana ilikuwa ya tatu.

Shule ya Sekondari ya Kibaha (Pwani) imeshika nafasi ya tano wakati mwaka jana ilishika nafasi ya tisa. Kisimiri (Arusha) imekuwa ya tatu ilhali mwaka jana ilikuwa ya tano kitaifa.

Shule zilizokuwa 10 bora mwaka jana lakini mwaka huu hazimo katika nafasi hiyo ni; Mzumbe (Morogoro) iliyokuwa ya pili, Ilboru Arusha (4) na Mtakatifu Mary Mazinde Juu ya Tanga (6).

Nyingine ni Tabora Girls (7) na Kifungilo Girls ya Tanga iliyoshika nafasi ya 10.

Katika kinyang’anyiro hicho, shule zilizochukua nafasi ya shule zilizong’olewa katika kumi bora na nyingine kupanda kutoka nafasi moja hadi nyingine ni Igowole (Iringa) iliyoshika nafasi ya kwanza mwaka huu na mwaka jana ilikuwa ya nane. Iwawa (Njombe) imeshika nafasi ya nne. Nyingine ni Nangwa (Manyara) nafasi ya saba, Uwata (Mbeya-8), Kibondo (Kigoma-9) na Kawawa (Iringa) imefunga ukurasa kwa kuwa ya kumi.

Shule zilizokuwa za mwisho mwaka jana katika kundi la wanafunzi chini ya 30 na zaidi ya 30 mwaka huu licha ya mabadiliko hayo ni shule tatu ziliyobaki na nyingine maarufu zikiingia kwa mara ya kwanza.

Baadhi ya shule zilizoshika mkia ni Fidel Castro (Pemba), Tambaza (Dar es Salaam), Muheza (Tanga), Mtwara Technical (Mtwara) na Iyunga Technical ya Mbeya. Al-Falaah Muslim (Unguja) na Osward Mang’ombe (Mara) zikiingia kwa mwaka wa pili mfululizo.



SHULE 10 ZILIZOONGOZA

1. Igowole
2. Feza Boys 
3. Kisimiri
4. Iwawa
5. Kibaha
6. Marian Girls
7. Nangwa
8. Uwata
9. Kibondo
10. Kawawa

MWANAFUNZI MWENYE MIAKA 6 ABAKWA NA MWALIMU PAMOJA NA MLINZI

Polisi Kusini mwa India wamesajili kesi ya ubakaji ambapo inaarifiwa mtoto wa shule mwenye umri wa miaka 6 alibakwa na wafanyakazi wawili wa shule moja maarufu mjini Bangaloer.
Kisa hicho kinaarifiwa kutokea wiki mbili zilizopita. Mtoto huyo alibakwa na mlinzi pamoja na mwalimu, lakini kwa sababu ya kuwepo walinzi wengi katika shule hiyo, polisi bado wanachukua muda kuchunguza mlinzi aliyehusika.
Polisi wanasema kuwa mtoto huyo alibakwa tarehe mbili Julai , lakini wazazi wake waligundua hilo siku chache zilizopita baada ya mtoto huyo kulalamika kuumwa na tumbo na kupelekwa hospitalini.
Wakati huo mamia ya wazazi wameandamana nje ya shule wakivunja milango na kupiga mayowe kulaani tukio hilo.
Polisi tayari wamesajili kesi hiyo , lakini bado hawajamkamata mtu yeyote.
Mwandishi wa BBC Andrew North mjini Delhi anasema kuwa tukio hilo ni la hivi karibuni kugonga vichwa vya habari nchini India.
Waziri mkuu Narendra Modi, ameahidi kupambana vilivyo na visa vya ubakaji, na udhalilishaji wa kijinsia , lakini unyanyasaji wa wanawake bado ni tatizo kubwa sana nchini humo.
Huku taarifa ya kubakwa kwa mtoto huyo zikijitokeza tu, mamia ya wazazi walikusanyika nje ya shule hiyo na kutaka hatua kuchukuliwa dhidi ya wasimamizi wa shule.
Mnamo siku ya Alhamisi mwenyekiti wa shule Rustom Kerawala alizungumza na wazazi ambapo aliomba msamaha na kuahidi kushirikiana na polisi katika uchunguzi.

JACKLINE WOLPER AFUNGUKA YOTE KUHUSU YEYE NA NEY WAMITEGO SOMA HAPA KUJUA ALICHOSEMA PATA STORI HAPA

Huko Instagram kuna Jamaa Anajiita Dougiemasta13 sijui Siwema ambae ni mchumba wa Nay wa Mitego kamkosea nini Maana madogo anayomshushia...Duuuhhh ...Baada ya Jana Kuweka Video ya Wema akivishwa pete na Jamaa mwingine leo Kaja na Mpya....


JIONEEE..... 


HUJAFA HUJAUMBIKA, ONA MREMBO HUYU ANAVYOTESEKA NA GONJWA LA AJABU

Dada Zuhura Juma (27) mkazi wa Temeke jijini Dar.Stori: IMELDA MTEMA NA MAKONGORO OGING’

HAWAKUJUA kama wangekuwa hivi, lakini imetokea tu! Zuhura Juma (27) mkazi wa Temeke jijini Dar na Disnia Rajab, mwenye makazi yake Gezaulole jijini Tanga, wapo katika mateso makali kwa muda wa miaka kumi sasa baada ya miguu yao kuvimba kwa namna ya kusikitisha.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa gazeti hili, wanawake hao walisema walipatwa na ugonjwa huo bila kutarajia. Awali walianza kuhisi maumivu ya kawaida na kuamini wangepona, lakini miguu yao iliendelea kuvimba siku baada ya siku.

Dada Disnia Rajab mkazi wa Gezaulole jijini Tanga.

Akisimulia mkasa wake, Zuhura alisema ugonjwa huo ulimpata mwaka 2004 alipopata ujauzito wa mtoto wake wa kwanza.
Dada Disnia Rajab kabla ya kupata ugonjwa.

“Kwanza nilipata tatizo la presha ambayo ilisababisha miguu kuvimba lakini sikuwa na shaka kwani nilijua ni hali ya kawaida kwa mama mjamzito kuvimba miguu kisha hurejea katika hali ya kawaida.
“Baada tu ya kujifungua, mguu mmoja ulirudi kama kawaida lakini huu (wa kushoto) ukawa bado, nilipokwenda hospitali waliniambia nisijali utarudi wenyewe kama zamani.

“Wakaniambia niendelee kunywa vidonge vya Laxis walivyonipa kwa ajili ya kupunguza maji.
“Lakini cha ajabu, siku moja hali yangu ilizidi kuwa mbaya, nikaenda Hospitali ya Temeke. Wao walishindwa kunitibu na kunihamishia Muhimbili ambako nililazwa kwa muda wa siku tano,” alisema.

Aliongeza kuwa, baada ya kuruhusiwa kurejea nyumbani, alianzishiwa kliniki ya ugonjwa wa matende iliyopo Muhimbili lakini katika hali ya kusikitisha madaktari walimwambia hawezi kutibiwa nchini.
“Kwa kweli nililia kwa uchungu maana nilijua uwezo wa kwenda huko nje ya nchi sina, nikaona nakufa na urembo wangu.”

Kwa upande wake, Disnia alisema yeye pia aliupata ugonjwa huo mwaka 2004. Kwanza alihisi maumivu ya kichwa ghafla usiku huku mwili ukitoka jasho. Asubuhi kulipokucha, alikuta mwili umevimba.
“Nilichukuliwa hadi Hospitali ya Bombo. Pale nililazwa kwa siku saba, presha ilikuwa juu, nikawekewa dripu, nilichomwa sindano presha ikashuka. Uvimbe wa mwili ukapungua isipokuwa mguu huu wa kushoto, madaktari waliniruhusu kurudi nyumbani ili nianze kliniki,” alisema.

Alisema pamoja na kuanza kliniki, hali ikazidi kuwa mbaya. Amezunguka hospitali nyingi na kutibiwa, lakini kote huko imeshindikana hadi alipoambiwa asingeweza kutibiwa nchini na anatakiwa kuwa na fedha kiasi kisichopungua shilingi milioni 20.

Licha ya matatizo ya maumivu yanayomfanya asiwe na uwezo wa kujitafutia riziki, pia watoto wake watatu aliozaa na mumewe aliyemkimbia baada ya kupatwa na ugonjwa huo, wamekuwa wakimtegemea yeye.

WANACHOOMBA KWA WATANZANIA
Kama kuna Mtanzania yeyote aliyeguswa na matatizo ya wanawake hawa, anaombwa kutoa aina yoyote ya msaada anaoona unafaa huku ikizingatiwa kuwa, kutoa ni moyo na si utajiri.
Kwa Zuhura Juma, tumia simu namba 0754 021301 au 0717 319555 na kwa Disnia Rajab, wasiliana naye kwa simu namba 0755 033718, 0685 836159 au 0719 546505.

FLORA MBASHA NA MUMEWE BADO NDOA YAO IPO KATIKA VURUGU KUBWA

Imebainika  kwamba  waimbaji  wa  muziki  wa  Injili  nchini, Flora Mbasha  na  mumewe, Emmanuel  Mbasha  hawajapatana  kama ilivyodaiwa  awali  na  taarifa  zinasema  kuwa  mwanadada  huyo  ameanza  maisha  yake  kivyake  kwa  kupanga  nyumba  nyingine  mbali  na  mumewe….
 
Habari  za  kuaminika  toka  ndani  ya  familia  ya  Flora  zinasema  kuwa  msanii  huyo  amekuwa  na  wakati mgumu  wa  kumsamehe  mumewe  kutokana  na  tabia  zake  chafu  ambazo  zimekuwa  zikiutesa  moyo  wake  na  sasa  anang’ang’ania  kumchukua  mwanaye…..
 
“Hivi  karibuni  iliripotiwa  kuwa  wanandoa  hao  wamepatana  lakini  ukweli  ni  kwamba  hakuna  kitu  kama hicho,mwanamke  amepanga  chumba  chake  hapa  Dar  es  Salaam  na  kumwachia  kila  kitu  mumewe  ambaye  sasa  ana haha  kumchukua  mwanaye  ili  aishi  naye,” kilisema  chanzo  cha  habari.
 
Lakini  upande  wa  pili, mume  wa  msanii  huyo  hivi  karibuni  alieleza  kuwa  ugomvi  baina  yao  ulianza  kutokana  na  kuchepuka  kwa  mkewe, huku  akipeleka  shutuma  kwa  mchungaji  wa  kanisa  la  ufufuo  na  Uzima, Josephat  Gwajima  ambaye  ni  maarufu  kwa  vitu  ambavyo  ni  tofauti  na  huduma  zake….
mbasha
Emmanuel  Mbasha  tayari  alishatoa  waraka  wa  wazi  kwenda  kwa  mchungaji  huyo, akimtaka  kukaa  mbali  na  ndoa  yake  jambo  ambalo  bado  halina  mrejesho  chanya  kwani  wawili  hao  Flora  na  Gwajima  wameendelea  kufanya  kazi  pamoja  kitu  kinachopelekea  Emmanuel  kuona  bado  kuna  kitu  kinaendelea  kati  yao….
 
Kutokana  na  hali  hiyo, mume  wa  Flora  amekuwa  mgumu  kumtoa  mtoto  wake  akihofia  kulelewa  na  mtu  ambaye  kwake  anamchukulia  kama  adui  wa  familia  yake…
 
“Imekuwa  ngumu  sana  kwa  Emmanuel  kumwachia  mtoto  wake  katika  hali  hii, hata  kama  ni  wewe  unamuachiaje  mtoto  wako  kipenzi  aende  kwa  mwanamke  ambaye  ni  msaliti,” alisema  ndugu  wa  karibu  wa  Emmanuel  Mbasha
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger