MKUTANO WA BONGO MOVIES NA BONGO FLEVA TIMBWILI LAIBUKA
JAZBA
baab’kubwa imeibuka katika mkutano wa wasanii wa filamu za Bongo ‘Bongo
Movies’ na Bongo Fleva ulioandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
kwa kushirikiana na chombo cha kusimamia haki za wasanii nchini,
Cosota.
Jacob Steven ‘JB’.
Tukio hilo lilijiri Jumatatu iliyopita ndani ya Ukumbi wa Vijana
Social, Kinondoni, Dar ambapo mastaa wa filamu, Jacob Steven ‘JB’ na
Issa Mussa ‘Cluod 112’ waliihoji Cosota juu ya tatizo la wizi wa kazi za
wasanii ndipo ‘kiliponuka’ baada ya kutoridhishwa na majibu.
Issa Mussa ‘Cluod 112’.
Hali hiyo ilisababisha baadhi ya wasanii, wakiwemo JB na Cloud kutoka
kikaoni na kuendelea na mambo yao mengine huku wawakilishi wa TRA
wakiendelea na kikao na kufafanua mipango yao.