Muigizaji wa filamu, Rose Ndauka amejifungua mtoto wa kike Jumapili iliyopita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam na kusisitiza, amefanana na baba yake.
Ndauka ambaye miezi michache iliyopita, alitangaza kusimama kuigiza kwa muda wa mwaka mmoja ili ajitathmini alijifungua mtoto huyo kwa operesheni.
Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti, Ndauka alisema: “Namshukuru Mungu, nimefanikiwa kujifungua salama, mtoto mwanamke.Ni faraja kwangu kwa sababu nimepata mwenzangu na amefanana na baba yake mzazi,” alisema Ndauka.
Ndauka ni mwigizaji maarufu wa filamu anayekubalika katika tasnia hiyo huku akitamba na kazi zake mbalimbali zikiwamo, Bad Girl, Fall in Love na nyinginezo.
Source: Mwanaspoti.